BETI NASI UTAJIRIKE

BONDIA ANTONY JOSHUA ALIPA KISASI KWA ANDY RUIZ

Mwanamasumbwi uzito wa kati Antony Joshua amefanikiwa kulipa kisasi baada ya kupokea kipondo kwenye  mchezo wa kwanza. Kupitia mchezo huo  Antony Joshua alipambana  na alifanikiwa  kurejesha mikanda yake ya WBO, IBF, WBA na IBO. Andy Ruiz Jr ameomba pambano la tatu na Joshua amesema yupo tayari. Huku akimpiga Ruiz Andy kwa pointi kwenye mchezo huo uliofanyika dimba la Adi Diriyah nchini Saudi Arabia .
Kwenye mchezo huo Joshua alishinda kwa pointi 118-110, 118-110 na 119-109 zote akiongoza. Kwa upande wapili Bondia wa Tanzania Seleman Said amepigwa kwa KO round ya kwanza na bondia kutoka USA Diego Pacheco katika pambano la round 4  la utangulizi kabla ya pambano la Anthony Joshua na Andy Ruiz kuanza

Post a Comment

0 Comments