BETI NASI UTAJIRIKE

BAADA YA ZAHERA KURUDI DAR, ZENGWE LAANZA JANGWANI

Klabu ya Yanga imejikuta  ikipunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.


Matokeo hayo yameiongezea kila timu pointi moja na naifanya Yanga SC ifikishe pointi 17 katika mchezo wa nane na kujivuta hadi nafasi ya tisa, wakati KMC inafikisha pointi tisa katika mchezo wa 11 na inashika nafasi ya 17 kwenye Ligi Kuu ya timu 20.


Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza katika mchezo wa leo, Yanga SC ilitangulia kwa bao kiungo mshambuliaji mkongwe, Mrisho Khalfan Ngassa ‘Uncle’ aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mnamibia, Sadney Urikhob. 


Ngassa alifunga bao hilo kiufundi dakika ya 73 akimchambua kipa namba moja wa timu ya taifa ya Burundi, Jonathan Nahimana akimalizia pasi nzuri ya kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Sibomana.

Beki mkongwe wa Yanga, Kelvin Patrick Yondan akamuangusha kwenye boksi kiungo mshambuliaji mwenye kasi wa KMC, Hassan Salum Kabunda na refa Heri Sasi akaweka penalti ambayo ilifungwa kiufundi na kiungo Abdul Hilary kufanya mchezo uishe 1-1.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, bao pekee la Bright Obina dakika ya 72 lilitosha kuipa Biashara United ushindi wa 1-0 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.

Biashara United inafikisha pointi 15 katika mchezo wa 13 ingawa inabaki nafasi ya 15 na Ndanda FC inabaki nafasi ya 18 na pointi zake nane baada ya kucheza mechi 13 pia.
 
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Farouk Shikharo, Juma Abdul, Jaffar Mohamed, Lamine Moro, Kelvin Yondan, Ally Mtoni ‘Sonso’/Mapinduzi Balama dk70, Deus Kaseke, Papy Kabamba Tshishimbi, David Molinga, Sadney Urikhob/Mrisho Ngasa dk46 na Patrick Sibomana.

KMC; Jonathan Nahimana, Kelvin Kijiri, Ally Ramadhani, Ismail Gambo, Abdallah Mfuko, Kenny Ally, Rayman Mgungila, Mohamed Samatta/Abdul Hilary dk49, Ramadhani Kapera, Hassan Kabunda na Serge Noguez/Aaron Lulambo dk76.

Post a Comment

0 Comments