BETI NASI UTAJIRIKE

BAADA YA SIMBA KUMTAMBULISHA KOCHA MBELGIJI , YANGA INALETA KOCHA MZAWA

Klabu ya Yanga inapambana  kumalizana na Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime kwa ajili ya kuliboresha benchi lao la ufundi, huku mwenyewe akisubiri kwa hamu


Maxime ni kati ya makocha waliokuwa wakipambanishwa katika nafasi hiyo ya kocha msaidizi pamoja na Kally Ongala aliyewahi kuichezea timu hiyo na kuifundisha Azam FC.

Yanga inataka kumpa kibarua Maxime ikiwa ni siku chache tangu uongozi wa timu hiyo kulivunja benchi zima la ufundi akiwemo aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mkongomani, Mwinyi Zahera.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata www.amospoti.com uongozi wa timu hiyo tayari umewasiliana na kocha huyo kwa ajili ya kufanya mazungumzo ili kuhakikisha anatua Yanga.

“Kila kitu kinakwenda vizuri kati yetu viongozi na kocha Maxime ni baada ya jina kupitishwa kati ya majina mawili yaliyokuwepo mezani yakijadiliwa akiwemo Kally aliyewahi kuichezea Yanga.

“Maxime ni kati ya makocha waliofanya vizuri katika misimu hii mitatu ukiwemo huu baada ya kuiwezesha timu yake kuwepo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 24, huku Simba ikiongoza ikiwa na 25,” alisema mtoa taarifa huyo.

Maxime yupo mapumzikoni mkoani Morogoro baada ya ligi kusimama kupisha michuano ya Chalenji, amekiri kuzungumza na mabosi hao wa Yanga lakini bado hawajafikia mwafaka.

“Kweli kabisa viongozi wa Yanga walinitafuta, lakini bado tunazungumza kama tutakubaliana nitakuja Dar es Salaam kukamilisha masuala mengine,” alisema Maxime.

Post a Comment

0 Comments