BETI NASI UTAJIRIKE

BAADA YA SADNEY NA BALINYA KUONDOKA MCHEZAJI MWINGINE ATARAJIWA KUONDOKA YANGA

Mwaka 2019 utakumbukwa kwa mengi hasa kwa klabu ya Yanga kuendelea kupata wakati mgumu kwa mambo mbalimbali yanayoendelea klabuni hapo. Machache ya mambo 


hayo ni Maendeleo yaliyofanywa na wapinzani wao Simba kwa kumiliki viwanja vya kisasa vya mazoezi huku wao wakikosa mishahara kwa wachezaji na kupelekea baadhi yao kuvunja mikataba. 

Jingine tena limeibuka klabuni hapo baada ya mchezaji mkongwe wa klabu ya Yanga, Mrisho Ngassa kuzua hofu kubwa mitandaoni kufuatia kauli yake aliyoiandika kunako mtandao wake wa Instagram.

Ngassa aliandika maelezo ambayo yaliwachanganya wengi na kuwafanya kutafakari juu ya kauli yake ambapo wengi walionekana kuamini kuwa anaondoka na wengine wakiwa hawaielewi.Hiki ndicho alichokiandika Ngassa kunako ukurasa wao wa Instagram.Post a Comment

0 Comments