Kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi amejiudhuru rasmi kuifundisha timu hiyo baada ya mwenendo mbaya wa matokeo kwa Klabu hiyo.
Inasemekana Mwalimu Mambusi aliandika barua ya kujihudhuru tangu November 26 kwa madai ya kulinda maslahi ya klabu baada ya kuiongoza klabu hiyo katika michezo 12 na kushinda mchezo 1 kusuluhu 5 na kupoteza michezo 6.
Uongozi wa Mbeya City umeikabidhi timu hiyo kwa Kocha msaidizi Mohammed Kijuso mpaka pale mchakato wa kumpata Kocha mwingine utakapofanyika.
Toa maoni yako kuhusiana na wimbi la makocha Kutimuliwa au kuachana na vilabu vyao.
0 Comments