BETI NASI UTAJIRIKE

ARSENAL MICHOSHO TU WAMEPIGWA TENA

Klabu ya Arsenal imeendelea kuwa na wakati mgumu ligi kuu Uigereza baada ya kuruhusu kipigo kingine kutoka kwa Brighton na kuifanya timu hiyo kufikia rekodi ya kushinda mechi 4


 tu huku ikitoka sare mechi 7 n kufungwa 4. Arsenal imeendelea kuwa na wakati mgumu mbali na kumtimua kocha wake Unai Emery wakidhani alikosa mbinu za kufundishia lakini ujio wa kocha wa muda Ljungberg bado umeonyesha wachezaji wa klabu hiyo ndiyo majanga zaidi.

Ljungberg alikabidhiwa timu hiyo na amefanikiwa kuiongoza timu hiyo kwenye michezo miwili akiambulia kupata pointi moja pekee kati ya 6. Mchezo wake wa kwanza ulikuwa ni dhidi ya Norwich City uliomalizika kw sare ya mabao 2-2 huku mchezo wa pili ni dhidi ya Brighton uliomalizika kwa sare ya mabao 2-1.

Kwa matokeo hayo Arsenal imeendelea kubaki nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi Iikiwa na pointi 19 na mchezo unaofuata ni dhidi ya Westham kisha Manchester City.  Kwa sasa hata aje Guardila au Mourinho pamoja na Zidane bado timu hiyo itakuwa ni nyepesi kufungwa kwani wachezaji wake wamekwishakufa moyo wa kujituma na kufanya vizuri.

Post a Comment

0 Comments