BETI NASI UTAJIRIKE

ANTONIO NUGAZ NA HAJI MANARA WAUNGANA KUMLILIA MZEE AKILIMALI

Klabu ya Yanga imeondokewa na aliyekuwa katibu mkuu barza la wazee mzee Ibrahimu Akilimali aliyefariki alfajiri ya leo. Mzee akilimali amekuwa ni  nguzo muhimu kwenye uongozi wa Yanga. 


Kifo cha Mze Akilimali kimeibua hisia miongoni mwa mashabiki wa soka nchini  akiwemo msemaji wa Simba bwana Haji Manara alieandika 

"Tumeondokewa, Mwamba katika Miamba ya kabumbu Nchini umeanguka,Mzee wetu,Baba na Babu yetu, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Yanga Ibrahim Akilimali katangulia mbele ya haki, poleni Familia, poleni Wanayanga,huu ni msiba wetu sote na tutashiriki kikamilifu kwenye majonzi haya”

Mhamasishaji wa Yanga Bwana Antonio Nugaz ameumizwa na kifo cha nguli huyo wa soka nchini na alinukuliwa kwa kuandika 

"Nimepokea kwa mstuko taarifa za kifo Cha aliyekuwa shabiki na mwanachama wa Yanga Mzee Ibrahim Akilimali ambacho kimetokea Nyumbani kwake Bagamoyo, Mzee Ibrahim Akilimali ambaye amepatwa na umauti Bagamoyo maziko ni kesho saa 10 alasiri Tandale kwa Mtogole,inaah lillah wainnah ilayh rajiuun..Allah amlaze mahala anapo stahi". 

Post a Comment

0 Comments