Aliyekuwa kocha wa Juventus ya Italia Massimiliano Allegri anaamini staili ya uchezaji iliyoletwa na Guardiola akiwa Barcelona si ya kila timu kuicheza. Kocha huyo mkongwe
amenukuliwa akisema " Philosofi ya Pep Guardiola ya kucheza mpira wa tiki-taka iliyochezwa na barcelona toka mwaka 2008-2012 si ya kila timu. Staili ile iliwafanya wachezaji watatu Messi,Xavi na Iniesta kuipa mafanikio makubwa klabu hiyo kwa kutwaa vikombe 14 kwa kipindi kifupi"
" Baadhi yetu tulifuata staili ya Guadiola kwa miaka 20 lakini aina ile ya mpira si kwa kila mtu . Binafsi napenda kucheza mipira ya Kaunta Ataki na imenipa mafanikio"
Guardiola aliondoka Barcelona msimu wa 2013 na alihamia Bayern Munich ana mwaka 2016 alijiunga na Manchester City na sasa anaendelea kuinoa klabu hiyo.
Awali ilitabiriwa aina ya uchezeshaji timu wa Guardiola ungeshindwa kufanikiwa akiwa Manchester City lakini kocha huyo amebadili mitazamo ya wachambuzi mbali mbali huku kila mtu akitamani timu yake icheze kama Mancester City.
0 Comments