BETI NASI UTAJIRIKE

AHADI MBILI ALIZOZITOA KOCHA MPYA WA SIMBA SVEN VANDERBROECK

Kocha mkuu Sven Vanderbroeck ameonekana kufufurahishwa kujiunga na mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania klabu ya Simba.Kocha huyo aliyetambulishwa hapo juzi 


ametoa ahadi kadhaa kuelekea kuanza kuitumikia klabu hiyo. Kocha huyo alitambulishwa kwa viongozi na wachezaji wa Simba na baadaye alifanya mahojiano na Simba TV ambapo alinukuliwa akisema 

Lengo la kwanza ni kushinda ubingwa wa Ligi Kuu. Nataka kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, nataka kucheza mashindano ya CAF. Nataka Simba iwe kwenye hatua kubwa na kupata matokeo mazuri,
“Kilichonivutia Simba cha kwanza ni uwingi wa mashabiki. Ni jambo la kufurahisha kuona mashabiki 60,000 wakikushangilia inakupa hisia za kipekee”

Kocha huyo ataanza na mechi ya tarehe 25 Disemba dhidi ya Lipuli akifuatiwa na mchezo wa tarehe 28 dhidi ya KMC na tarehe 4-  Januari dhidi ya Yanga. 

Post a Comment

0 Comments