BETI NASI UTAJIRIKE

ACHANA NA UWANJA WA BUNJU SIMBA KUFANYA KUFULU NYINGINE DIRISHA DOGO

Klabu ya Simba inaendelea kuwavuruga wapinzani wake kwa kuwafunga njee na ndani ya uwanja. Klabu hiyo inajiandaa kumwaga mabilioni mengine kuanzia disemba 16 2019


Klabu hiyo kwa sasa imeamua kufanya mapinduzi ya kisoka na Katika kukiongezea makali kikosi cha Simba kunako safu ya ushambuliaji, inaelezwa mabosi wa klabu hiyo wako kwenye mchakato wa kuongeza winga mmoja wa nguvu.

Mkongomani Rossein Tuisila Kisinda anayekipiga AS Vita ya Congo, anatajwa kuwa katika rada za mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara na kuna uwezekano akashushwa hapa nchini dirisha dogo.

Kisinda ni straika anayecheza kama winga na inaelezwa amekuwa akiwaniwa na baadhi ya timu zingine nje ya Congo ili kupata huduma yake.

Mabosi wa Simba wanavutia zaidi nguvu kwa winga huyo huku mchezaji mwingine ambaye bado bado jina lake halijafahamika ni kutoka KCCA ya Uganda.

Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa Disemba 16 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments