ZIFAHAMU SABABU TATU ZA UNAI EMERY KUTIMULIWA ARSENAL

Klabu ya Arsenal imetangaza rasmi kuachana na aliyekuwa kocha wake Unai Emery. Tangu kuanza kwa msimu wa 2019/20 klabu hiyo imeshindwa kufanya vyema kwa kushinda 



michezo 5 tu kati ya 13 iliyocheza ligi kuu Uingereza huku ikifungwa 4 na sare 4 na kuifanya kujikusanyia pointi 19 huku ikiwa nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi . Hizi hapa sababu za Arsenal  kumfukuza Unai Emery

1. Kushindwa kufuzu ligi ya mabingwa Ulaya 

Arsenal ilijiwekea utamaduni wa kumaliza ligi ikiwa ndani ya nne bora ila tangu kuondoka kwa kocha wake mkongwe Arsene Wenger wameshindwa kufuzu hatua hiyo na kuifanya kucheza misimu 4 ya ligi kuu bila kushiriki UEFA. Msimu wa 2018/19 klabu hiy ilifuzu kucheza fainali za Europa dhidi ya Chelsea lakini ilipoteza mchezo huo. Kama ingetwaa kombe hilo basi ingefuzu moja kwa moja ligi ya mabingwa ulaya .

2. Michezo 7 bila ya ushindi 

Mashabiki wa Arsenal walianza kususia kwenda uwanja wa Emirates na sababu kubwa ilikuwa timu hiyo kufanya vibaya . Arsenal ilipata ushindi wake wa mwisho kwenye ligi kuu Uingereza dhidi ya Bournemouth tarehe 6 Octoba waliposhinda bao 1-0. Klabu hiyo imeondolewa kombe la ligi kwa kufungwa na Liverpool. Mashabiki hao walionyesha hasira zao kwenye mchezo wa Europa dhidi ya Eintraicht kwa kuhudhulia kiwango kidogo zaidi na timu hiyo kufungwa mabao 2-1

3.Kutotumia baadhi ya nyota wa klabu hiyo

Emery aliingia katika mgogolo na mchezaji ghali zaidi klabuni hapo Mesuit Ozil. Kupitia uggomvi huo Emery amekuwa akimweka nje ya Uwanja nyota huyo tangu kuanza kwa msimu na kumfanya ashuke kiwango. Kutotuka kwa ozil kumeleta matokeo mabovu zaidi klabuni hapo. Msimu huu wa 2019/20 unafananishwa na msimu wa 1991/92 kwa klabu hiyo

Post a Comment

0 Comments