advertise with us

ADVERTISE HERE

ZAHERA AZUNGUMZA MWANZO MWISHO UNAFIKI WA YANGA NA SABABU ZA KUONDOLEWA KWAKE

Aliyekuwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amefunguka kilichomfanya akatimuliwa na klabu ya Yanga . Sababu kubwa ya kocha huyo kuondoka ni unafiki wa mtu afahamikae kwa jina 





la Ndama.   Zahera amenukuliwa akisema "Mwenyekiti wa Yanga aliniambia kocha Noel Mwandila anatakiwa kuondoka na nafasi yake ichukuliwe na Charles Boniface Mkwasa. Nikawakatalia kwakuwa ni Kocha Mkubwa aliyewahi kufundisha timu ya Taifa hawezi kuwa msaidizi, itakuwa vigumu kumpa maagizo. Nikawaambia kama Kocha msaidizi waniachie mimi nimtafute mwenyewe"
"Boss wako akikuambia nakata mkataba wako utaweza kumwambia hapana huwezi mimi nabakia hapa?, kama wameamua nasubiri barua waseme sababu na mimi nitajibu maswali yote, Yanga hawakunipa target ya kwamba lazima kuingia hatua ya makundi kombe la shirikisho au Klabu bingwa mkataba wangu hausemi hivyo, nilikua na mkataba na wote mnajua mkataba ukivujwa unatakiwa kudai pesa"
"Kule Mwanza wakati tunajiandaa kucheza na Pyramids Viongozi walituweka kwenye Hotel ya kwenye Mtaa kama wa Kariakoo Ikabidi niombe namba ya Boss wa GSM ambaye alikuwa Dubai nikazungumza naye na kumueleza juu ya sehemu tuliyofikia akaniuliza kweli Coach mmefikia hapo? Kesho yake akatusaidia tukahama Hotel na kwenda Hotel nzuri. Namshukuru sana Boss wa GSM"
"Suala la beki Vicent Dante kugoma kujiunga na timu mpaka alipwe pesa zake alikuwa yupo sawa maana zile pesa zilizochangwa kwenye kubwa kuliko ilitakiwa zilipe kwanza madeni ya wachezaji ambao walikuwa wanadai pesa zao za usajili, ila uongozi kuanza kuwalipa wachezaji wapya sio sawa maana wachezaji wa zamani wao ndio walitoa wazo la kuchangisha pesa zile."
"Wachezaji wa Yanga walikuwa wanakula mlo mmoja wakati mwingine ilikuwa inawapa ngumu wachezaji kupambana uwanjani na fedha zote nilizokuwa nazitoa kuisaidia Yanga zilikuwa za makubaliano ya kurudishiwa baada ya Yanga kuvunja mkataba na mimi naamini uongozi wa Yanga utafanya haraka kurudisha fedha zangu zote ambazo nilizitoa kusaidia timu"


Post a Comment

0 Comments