advertise with us

ADVERTISE HERE

YANGA,AZAM ZAANZA KUMMENDEA MWAMBA WA LUSAKA (CHAMA)

Kiungo wa klabu ya Simba na timu ya taifa Zambia Clatous Chama amegeuka dili kwa vilabu vya Azam na Yanga baada ya kukosa nafasi ya uhakika kikosi cha kwanza Simba 


Kwa msimu wa 2019/20 Chama ameonekana kucheza chini ya kiwango kulinganisha na msimu wa 2018/19 ambao alijiunga na mabingwa hao watetezi na kuonyesha uwezo wa hali ya juu sana hasa mechi za kimataifa na kujihakikishia nafasi kikosi cha kwanza .

Msimu huu mambo yamebadilika kwa upande wa nyota huyo kwani amekuwa akitokea  benchi huku nafasi yake ikigombewa na wachezaji watatu akiwemo Ajib na Shiboub. 

Kukosekana kikosi cha kwanza kwa mchezaji huyo kumezifanya klabu za Yanga na Azam kuanza kumtolea macho. Taarifa zisizo rasmi zinasema Azam FC wameandaa dau nono kunasa saini ya kiungo huyo raia wa Zambia mwenye uwezo wa kipekee. Mbali na Azam kuonyesha nia lakini pia mabingwa wa kihistoria Yanga  wameonekana kuhitaji huduma ya kiungo huyo makini. Tetesi hizo zimezagaa ikiwa imesalia masaa machache tu dirisha dogo la usajili kufunguliwa.

Klabu ya Simba haijazungumzia chochote kuhusu hatma ya Chama tangu alipomalizana na kamati ya nidhamu mwezi uliopita kwa tuhuma za kutosafiri na wenzake kuelekea Kagera kwenye michezo ya Kagera Sugar na Biashara .

Amospoti.com inafuatilia kwa umakini kupata uhakika wa tetesi hizo 

Post a Comment

0 Comments