YANGA YATANGAZA KUUTUMIA MCHEZO DHIDI YA ALLIANCE KAMA SALAMU KWA SIMBA

Kuelekea mchezo wa ligi kuu jioni ya leo kati ya Alliance FC na Yanga mchezo utakaopigwa uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza klabu ya Yanga imeonyesha kutangaza kiama kwa 


Alliance.Yanga wamelielekeza benchi la ufundi na wachezaji kuwashukia Alliance kwelikweli jijini hapa kesho Ijumaa. Viongozi wamepania kipigo hicho cha sapraizi ili kuwashtua watani wao Simba wanaokutana nao Januari 4 mwakani.

Lakini vilevile kocha amewaahidi kutopoteza mchezo huo pamoja na kuwafanyia sapraizi Simba watakapokutana nao mwakani licha ya gharama ya vikosi hivyo kutofautiana.

Baada ya mchezo wa leo Ijumaa, Yanga itacheza tena tarehe 2 dhidi ya KMC na itapumzika mpaka itakapokutana na mwenyeji wao Simba kwenye Uwanja wa Taifa.

Mmoja wa vigogo wa ufundi wa Yanga, amesema kwamba kwenye mechi ya kesho wanaanzia kutafuta mzuka wa kuwavaa Simba na mambo mengi watafanya kimyakimya.

Boniface Mkwasa ambaye ni Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, amewasisitiza mashabiki waje uwanjani kwa kujiamini kwani Kirumba wameizoea na wanajua jinsi ya kuitumia kushinda mechi.

Kocha huyo ambaye akishinda atatimiza pointi tisa tangu akabidhiwe timu, amesema ataivaa Alliance kwa tahadhari kubwa kwa vile anajua watapania baada ya kipigo dhidi ya Azam.

Alliance wametoka kufungwa bao 5-0 na Azam katika hali ya kawaida lazima watukamie ili kupoza machungu yao na mimi nimejiandaa kuingia kwa tahadhari ili tuweze kupata matokeo katika mchezo huo, tuna kila sababu ya kushinda wala hatuhofii,” alisisitiza kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars ambaye ni mwanachama wa Yanga.

“Wote ni mashahidi kwamba tangu nipewe timu hii timu kiujumla imebadilika kiuchezaji hivyo nimejipanga kupambana ili pointi za Mwanza tusizipoteze, naamini tutapambana,” alisema na kuongeza kuwa CCM Kirumba hakumpi wasiwasi wowote.

“Kirumba hakutupi wasiwasi kwa kuwa naujua tangu nacheza hivyo mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kutusapoti tukiamini kwamba tutapata matokeo mbele ya Alliance,” alisema Mkwasa ambaye habari za ndani zinasema kwamba huenda akamaliza msimu Yanga.

Habari zinasema kwamba viongozi hawana mpango wa kubadili benchi la ufundi licha ya kupokea maombi kadhaa ya makocha kutoka ndani na nje ya nchi, Yanga wanaamini Mkwasa anatosha kwa ligi na FA.Yanga imekutana na Alliance mara mbili na kushinda zote. Dar mabao 3-0, huku Mwanza wakishinda bao 1-0.

Post a Comment

0 Comments