BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YAJIPANGA KUVITAFUNA VIPORO VYOTE LIGI KUU TANZANIA

Timu ya Yanga ambayo hadi sasa imecheza mechi sita tu za Ligi Kuu na kuwa na viporo vitano ili kufikia mechi 11 kama zilivyo timu nyingine zinazocheza michuano hiyo,


Wanajangwani hao watacheza mchezo wake wa kiporo dhidi ya Alliance kesho Novemba 29, kisha itapiga mwingine Desemba 2, dhidi ya KMC kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

Baada ya mechi zake mbili, Yanga na Simba zinatarajia kuendelea na ligi Januri 4, mwakani ambapo utakuwa ni mtanange wa wawili hao maarufu kama Kariakoo Derby 
kutokana na kusimama kwa michano hiyo, kupisha michuano ya Cecafa inayotarajia kufanyika Uganda.

Katika kipindi chote cha mwezi mmoja jeshi la kocha Boniface Mkwasa, litakuwa likijifua vilivyo kwa ajili ya mtanange huo, lakini pia ligi kwa ujumla.

Mkwasa baada ya kukiongoza kikosi chake kuwatungua JKT Tanzania mabao 3-2 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, aliwambia waandishi wa habari kuwa anatoa siku tatu pekee za mapumziko.

Baada ya mchezo huu tunatoa mapumziko ya siku tatu, Jumanne tunaanza mazoezi na kwa vile tutakuwa na muda mrefu wa kufanya mazoezi, tutajaribu kurekibisha mapungufu tuliyonayo, alisema.

Yanga ni timu pekee ambayo hadi sasa imecheza mechi chache zaidi (sita) na kufanikiwa kuvuna pointi 13 baada ya kupoteza moja dhidi ya Ruvu Shooting, sare moja mbele ya Polisi Tanzania na kutembeza vichapo kwa timu nyingine nne.

Post a Comment

0 Comments