BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YAINOGESHA KIGAMBONI KWA KUJIBU MAPIGO YA SIMBA

Klabu ya Simba hivi karibuni ilionyesha viwanja vyake viwili vya mazoezi vitakavyozinduliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT John Joseph Magufuli 


Klabu ya Yanga imeamua kujibu mapigo hayo ya klabu ya Simba kwa kuanza ujenzi wa viwanja vitatu vya mazoezi huko kigamboni.  Yanga walikabidhiwa rasmi hati ya eneo na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bw.Paulo Makonda mapema Oktoba na sasa wameshaanza kulisafisha eneo hilo. 


Klabu hiyo imetangaza kujenga viwanja vitatu vya mazoezi na itahusisha ujenzi wa hostel za wachezaji wa timu ya wanaume,timu ya wanawake na timu ya vijana. 

Mbali na klabu hiyo kutotoa taarifa kamili ya ujenzi  huo lakini picha zimevuja zikimwonyesha Injinia Bahati Mwaseba ambaye ni Mwenyekiti kamati ya ujenzi na mjumbe kamati ya utendaji akiwa site kukagua ujenzi huo



Muda si mrefu klabu hiyo itahama kutoka uwanja wake wa mazoezi Kaunda uliopo eneo la Jangwani na kuhamia Kigamboni eneo lililokubwa na watatumia kwa shughuli mbali mbali.

Post a Comment

0 Comments