BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YA MKWASA NI BALAA TUPU,WAENDELEA KUINYATIA SIMBA KIMYA KIMYA

Klabu ya Yanga imeendelea kufanya vizuri mechi zake za ligi kuu Tazania bara baada ya hapo jana kupata ushindi mwingine mnono dhidi ya  timu ngumu JKT Tanzania. Mabingwa 


wa kihistoria waliibuka kidedea kwa  kuichakaza JKT Tanzania 3-2  kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 13 katika mchezo wa sita na kupanda kutoka nafasi ya 15 hadi ya 12 sasa ikilingana kila kitu na Azam FC iliyopo nafasi ya 11 baada ya kucheza mechi saba.

Yanga SC iliuanza kwa kasi mchezo wa leo na kufanikiwa kupata bao lake la kwanza dakika ya 11, mfungaji Patrick Sibomana akimalizia krosi ya Deus Kaseke kufuatia shambulizi lilioanzishwa na beki Ally Abdulkarim Mtoni ‘Sonso’.


Lakini Adam Adam akaisawazishia JKT Tanzania dakika mbili tu baadaye akimtungua kipa Mkenya, Farouk Shikaro kwa shuti la juu baada ya kupokea pasi ya kiungo, Mwinyi Kazimoto.Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uganda misimu miwili mfululizo iliyopita, Juma Balinya akaifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 22 akimalizia pasi ya beki wa kulia Juma Abdul.

Mshambuliaji mpya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), David Molinga akaifungia Yanga SC bao la tatu dakika ya 35 kwa shuti la mpira wa adhabu baada ya Damas Makwaya kumchezea rafu Kaseke nje kidogo ya boksi.
Mshambuliaji Daniel Lyanga akategua mtego wa kuotea wa mabeki wa Yanga kuifungia JKT Tanzania nao la pili dakika ya 45 akimalizia pasi ya beki Adeyum Saleh Ahmed.


Kipindi cha pili Yanga SC walicheza kwa kujizuia kuruhusu bao lingine huku wakishambulia kwa tahadhari na wakafanikiwa kuvuna ushindi wa pili mfululizo chini ya kocha mpya na wa muda, Charles Boniface Mkwasa aliyechukua nafasi ya Mkongo, Mwinyi Zahera aliyefukuzwa mwanzoni mwa mwezi.


Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Farouk Shikaro, Juma Abdul, Jaffar Mohamed, Ally Mtoni ‘Sonso’, Lamine Moro, Papy Kabamba Tshishimbi, David Kaseke, Mapinduzi Balama/Mohamed Issa ‘Banka’ dk50, David Molinga/Abdulaziz Makame dk61, Juma Balinya na Patrick Sibomana/Mrisho Ngassa dk77.


JKT Tanzania;  Abdulrahman Mohamed, Michael Aidan, Adeyoum Ahmed, Frank Nchimbi, Damas Makwaya, Jabr Aziz, Mwinyi Kazimoto, Rchard Maranya/Hafidh Mussa dk64, Daniel Lyanga, Adam Adam/Anuary Kilemile dk83 na Edward Songo/Mohamed Rashid dk72.

Post a Comment

0 Comments