advertise with us

ADVERTISE HERE

WENYE KOMBE LETU TUMERUDI

Klabu ya Yanga imetangaza kurejea mbio za ubingwa baada ya kupata ushindi wa ugenini katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Ndanda FC 1-0 jioni ya leo Mchezo huo ulipigwa dimba la Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. 
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, nyota wa Rwanda Partrick Sibomana aliyefunga dakika ya 76 kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 20.

Refa Hance Mabena kutoka Tanga aliyekuwa anasaidiwa na Abdallah Rashid na Khalfan Sika wa Pwani aliamuru pigo hilo baada ya beki wa Ndanda FC, Aziz Sibo kuunawa mpira uliopigwa na Mrisho Ngassa nje kidogo ya boksi.


Kwa ushindi huo, Yanga SC iliyokuwa inacheza mechi ya kwanza chini ya kocha mpya na wa muda, Charles Boniface Mkwasa kufuatia kundolewa kwa Mkongo Mwinyi Zahera, inafikisha pointi 10 katika mchezo wa tano, sawa na Azam FC ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi. Post a Comment

0 Comments