advertise with us

ADVERTISE HERE

YANGA ILIVYOWASILI MTWARA , MKWASA AWA HABARI YA MJINI

Klabu ya Yanga iliondoka jana asubuhi jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani  Mtwara kwa ajili ya mechi ya ligi kuu Vodacom dhidi ya Ndanda FC mchezo utakaochezwa uwanja wa 
Nangwanda sijaona. Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa mwalimu Charles Boiface Mkwasa aliyekabidhiwa timu hiyo siku ya jumatatu baada ya klabu hiyo kutangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera. 

Mara baada ya kuwasili mashabiki wa timu hiyo wakazi wa mtwara walijitokeza kuipokea timu hiyo iliyotumia usafiri wa basi lao kutokea jijini Dar es salaam . Mapokezi yalifana na baadhi ya mashabiki kufurahishwa na maamuzi ya kumkabidhi timu kocha  Mkwasa. 


Wengi wanasubiri kuuona uwezo wake kwenye mechi dhidi ya Ndanda na wameonekana kumuamini sana kutokana na rekodi zake nzuri akiwa twiga stars na Taifa Starz.

Yanga imeenda Mtwara na kikosi cha wachezaji 20 na viongozi 7
Post a Comment

0 Comments