advertise with us

ADVERTISE HERE

WADAU WAMUONYA KOCHA MSAIDIZI TAIFA STARS KUHUSU MANULA

Mashabiki wa soka nchini Tanzania wamekerwa na kauli iliyotolewa na kocha msaidizi wa TAIFA stars kuhusu Manula


"Hatumchagui mtu kwa sura yake kwa sababu hatukuja kuposa sisi, Tunachagua mchezaji Mtanzania mwenye uwezo wa kucheza"

Hii kauli ya Kocha msaidizi wa timu ya Taifa Juma Mgunda kwa Aishi Manula sio ya kufurahia wala kuishabikia, inapaswa kupingwa vikali na mashabiki wa soka wote bila kujali ushabiki wetu wa vilabu.

Juma Mgunda kwa nafasi yake hakupaswa kutoa kauli Kama hii kwa Aishi Manula, kama anaona Aishi Manula kwa sasahivi hana kiwango au nafasi ya kuichezea timu ya Taifa  basi walau angeonyesha kumuheshimu na kuthamini mchango Ambao  Aishi Manula amewahi kuutoa katika timu ya Taifa,  Tukiacha ushabiki wetu, wote ni mashahidi, nyakati zote ambazo Manula amekuwa katika  majukumu ya timu ya Taifa, amekuwa akijitoa kwa moyo na maarifa yake yote kulitetea Taifa lake, 

Kauli Kama hii haifai kutamkwa kwa Manula na wachezaji wengine ambao wamekuwa wakivuja jasho na kukubali kujitoa kwa moyo na nguvu zao zote  na wakati mwingine mpaka kuumia kwaajili ya kulitetea Taifa lao.

Mgunda ni Kama baba au mzazi kwa Aishi, anapomtolea kauli Kama hii, haipendezi hata kidogo, kauli Kama hii inamvunja moyo na kumkatisha tamaa.

 Mgunda Kama anaona Aishi hivi sasa Hana nafasi  Kwenye kikosi cha timu ya Taifa, Basi asimtolee maneno mabaya kwani Manula bado ana Safari ndefu ya maisha ya soka, leo Mgunda anamuona Manula  hana nafasi Taifa Stars ila Kuna muda timu ya Taifa itakuja kumuhitaji Manula na atatakiwa kurudi kulitumikia Taifa lake.

Nani alijua Kama Juma Kaseja anaweza kuitwa tena timu ya Taifa na akawa msaada mkubwa kwa timu ya Taifa? Wakati wote tulikuwa tunaamini Juma Kaseja kwa umri wake ndio basi tena, tulojua ameisha na hatuwezi kumuona tena kwenye jezi ya timu ya Taifa.

Tujifunze kuweka akiba ya maneno kwa wachezaji wetu lakini hawa wachezaji ni binadamu kama tulivyo sisi sote, baadhi ya kauli zetu zinawaumiza Sana,

Post a Comment

0 Comments