Wachezaji wa Liverpool Joe Gomez na Jordan Henderson wameondolewa kambi ya Uingereza kuelekea mchezo utakaopigwa leo dhidi ya Kosovo kufuzu EURO 2020
Wachezaji hao wameondolewa kambini hapo . Gomez mwenye miaka 22 aliondolewa kambini hapo kwa majeraha kwenye kifundo cha mguu aliyoyapata akiwa mazoezini siku ya Ijumaa. Mbali na hilo mchezaji huyo alizomewa na mashabki wa Uingereza kwenye mchezo dhidi ya Montenegro kwa kusababisha Raheem Sterling kuondolewa kwenye kikosi hicho.
Kwa upande wa Henderson mcezaji huyo hakujumuishwa kwenye mchezo dhidi ya Montenegro waliyoshinda mabao 7-0 kwa sababu ya mafua. Nyota huyo amepata ruhusa ya kuondoka kambini hapo pia. Naye kocha wa timu hiyo ya taifa alinukuliwa akisema
"Wachezaji hao wameruhusiwa kurudi klabuni kwao hivyo basi kikosi chetu kitajumuishwa na wachezaji 23 tu "
Gomez na Henderson wanategemewa kuwepo kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Crystal Palace utakaochezwa tarehe 23 November.
0 Comments