ads

adds

WACHEZAJI 7 WAPYA SIMBA WASHINDWA KUTAMBA MBELE YA KMC

Klabu ya Simba jana jioni mchezo wake wa kirafiki dhidi ya KMC mchezo uliochezwa dimba la Chamazi na kushuhudiwa timu  hiyo ikipoteza mchezo huo kwa mabao 2-1. 

Simba ilikuwa ikiendelea na mazoezi yake ya kawaida baada ya wachezaji wake 11 kuitwa kuzitumikia timu zao za Taifa kwenye mechi za kirafiki na kufuzu AFCON 2021.

Kwenye kikosi hicho Simba ilitumia wachezaji wengi waliosajiliwa msimu huu wakiwemo wabrazil watatu ambao ni Da Silva , Wilker na Fraga huku wachezaji wengie wapya ni Deo Kanda,Kakolanya ,Ajib na Kahata.

KMC walipata mabao yake mawili kupitia Alli dakika ya 58 na 68 huku upande wa Simba wakipata bao la kufutia achozi kupitia Ibrahim Ajibu

Kocha wa timu hiyo Mberigiji Patrick Aussems bado anaendelea kuchambua wchezaji wa kikosi cha kwanza kutokana na klabu hiyo kujaza wachezaji wengi wenye vipaji .

Post a Comment

0 Comments