advertise with us

ADVERTISE HERE

UJUMBE WA HAJI MANARA AKIMUONYA KOCHA MKUU TAIFA STARS

Hisia za kila Mtanzania kwa sasa  zimehamia nchini Tunisia kwenye lile jiji la Tunis kuelekea mchezo wa pili wa kundi J kati ya Tanzania na wenyeji Libya. Mchezo huo wenye hisia kali

Kwa Watanzania utapigwa siku ya jumanne 19 Novemba. Stars inashika nafasi uya pili ya kundi J ikiwa na pointi 3 na goli 1 la faida huku Tunisia ikiongoza kundi hilo kwa pointi 3 na magoli 3 ya faida. Equatorial Guinea inashika nafasi ya 3 na nafasi ya nne inashikiliwa na Libya . 

Kuelekea mchezo huo wa kufuzu AFCON 2021 msemaji wa Simba na mjumbe wa kamati ya uhamasishaji Taifa Stars Haji Manara amemwandikia ujumbe wa wazi kocha Ettiene kuhusu tabia za mashabki hasa Watanzania

Mwalimu @etiennendayiragije unaweka kitu kwenye mioyo ya Watanzania now,Wenyewe huku Site washaanza kukuita Boss!!!
Nikuase "Boss" Washabiki wa mpira kote duniani ni vigeugeu ila unapaswa kucheza na akili zao bila kuathiri utaalam wako wa kiufundi!!
Shinda na akili zao na ikibidi kuloose, basi mloose wote!!
Soka waipendayo Wabongo ni ile ya Sukari guru but wape test tofauti kdogo, na waonyeshe kwa vitendo approach ya kucheza Taifa hailingani na utakavyocheza away na Libya!!
Nakuaminia na nnajua tarehe kumi na tisa utakuja na plan ya tafuta X
Nakuaminia "Boss"


Kocha huyo anapaswa kutumia mbinu mbadala kuhakikisha Stars inashinda mchezo huo kwa hali na mali ili kujiweka nafasi nzuri za kushiriki AFCON 2021

Post a Comment

0 Comments