BETI NASI UTAJIRIKE

HIZI HAPA TIMU ZILIZOFUZU HATUA YA MTOANO UEFA HUKU MABINGWA WATETEZI LIVERPOOL NA CHELSEA HALI TETE

Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya maarufu kama UEFA Champions league iliendelea siku ya jumanne na jumatano kwenye michezo ya raundi ya 5 huku tukishuhudia baadhi ya


timu kufuzu moja kwa moja hata ya mtoano huku timu nyingine zikingoja michezo ya mwisho hatu ya makundi ili ziweze kufuzu hatua hiyo. Klabu za Chelsea na Liverpool zinaweza kushindwa kufuzu hatua hiyo mbali na kwamba zipo katika nafasi nzuri.

Liverpool 
Mabingwa hawa watetezi wapo kundi E wakicheza michezo 5 wakishinda 3,sare 1 na kufungwa 1 huku wakijikusanyia pointi 10 . nafasi ya pili kundi hilo ni Napoli mwenye pointi 9 na nafasi ya tatu ni Redbul mwenye pointi 7. Timu hizi zote tatu zinanafasi ya kufuzu hatua ya mtoano na kinachosubiriwa ni michezo ya mwisho kati ya Liverpool vs Red Bull na Napoli vs Genk anayoichezea Mbwana Samata
Chelsea 
Mabingwa watetezi wa Europa league wapo kundi H wakicheza michezo 5 wakishinda 2 sare 2 na kufungwa 1 huku wakijikusanyia pointi 8 nyuma ya Ajax wenye pointi 10 na nafasi ya tatu ni Valencia wenye pointi 8. Timu hizi zote tatu zinanafasi ya kufuzu hatua ya mtoano na kinachosubiriwa ni michezo ya mwisho kati ya Chelsea vs Lille na Ajax vs Valencia .

Kinachongojewa kwa hamu ni mechi za mwisho za hatua ya makundi zitakazopigwa tarehe 10 disemba.huku timu zilizokwishafuzu ni 

🇪🇸 Real Madrid, Barcelona
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Tottenham, Man City
🇫🇷 Paris Saint-Germain
🇮🇹 Juventus
🇩🇪 Bayern Munich, RB Leipzig

Post a Comment

0 Comments