advertise with us

ADVERTISE HERE

THIERY HENRY ALAMBA MADILI MAKUBWA MAWILI

Aliyekuwa kocha msaidizi wa Ubelgiji Thiery Henry amegeuka dili baada ya kulamba mikataba mikubwa miwili mmoja ukiwa ni nafasi ya ukocha na mwingine ni ubaloziShirikisho la soka barani ulaya liliingia mkataba mwingine na kinywaji cha Heineken kama wadhamini wakuu wa michuano ya EURO 2020 na Ligi ya mabingwa Ulaya (UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2021-2024) Thiery Henry amechaguliwa kuwa balozi mkuu wa kinywaji hicho kwa kipindi chote cha udhamini .

 Henry amepata nafasi hiyo baada ya kuisaidia ufaransa  kushinda kombe la EURO 2000 na UEFA  mwaka 2008/09 akiwa na Barcelona.

Dili la pili ni kocha huyo amesaini mkataba wa kuifundisha klabu ya Montreal inayoshiriki ligi kuu Marekani (MLS) . Henry ataitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 2 na kama atafanya vizuri basi atapatiwa mkataba mrefu zaidi.

Post a Comment

0 Comments