BETI NASI UTAJIRIKE

THIAGO SILVA AMPIGAMKWARA MESSI, TUTAWAONYESHA SISI NI NANI

Mchezaji wa PSG na kapteni wa timu ya Taifa Brazil ameonekana hana hofu na Messi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Argentina vs Brazil.



Messi amerejea dimbani kwa mara ya kwanza tangu alipofungiwa na chama cha soka Amerika Kusini (CONMEBOL) kwa kosa la kukishutumu chama hicho kupokea rushwa kutoka Brazil ili timu hiyo itwae kombe la COPA AMERICA.

Messi alikishutumu chama hicho mara baada ya timu yake kupigwa mabao 3-1 na Brazil na kuwafanya wasifike fainali za michuano hiyo ambayo Brazil ilitwaa kombe hilo.

chama cha soka CONMEBOL kilimpiga faini Lionel Messi kiasi cha dola 50,000 na kumfungia asicheze michezo minne ya timu ya Taifa. Messi anarejea kucheza mchezo wa kimataifa dhidi ya wapinzani wake wakubwa Brazil na Thiago Silva ameonekana kufurahishwa na Lionel Messi kwenye mchezo huo.

Silva amenukuliwa akisema   " Tunafurahia uwepo wa Lionel Messi kwenye mchezo huo,Wao (Argentina ) watakuwa na staa wao Lionel Messi ila sisi tutakuwa bila staa wetu Neymar aliye majeruhi ila Brazil ni Brazil na tulidhihirisha hilo kwenye COPA AMERICA.Mchezo kati ya Brazil vs Argentina huwa 50:50 na huwa wa kuvutia sana ila tunaamini tutafanya vizuri zaidi yao"


Mchezo huo wa kirafiki utapigwa nchini Saudi Arabia siku ya Ijumaa na unategemewa kuwa ni mkali huku timu ya Argentina ikipambana kulipa kisasi cha kutolewa nusu fainali kombe la COPA AMERICA kwa kipigo cha mabao 3-1. Kwa upande wa Brazil wao watataka kuonyesha ubabe wao bila ya uwepo wa Neymar JR  aliyemajeruhi kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments