BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO TAREHE 24-11-2019

Mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 24, hatotia saini kandarasi ya £450,000 kwa wiki hadi pale atakapothibitisha kuwa mkufunzi Pep Guardiola atasalia katika klabu hiyo kwa kipindi cha muda mrefu. (Sun on Sunday)
Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anaamini hatowasajili wachezaji anaowalenga katika dierisha la uhamisho la mwezi Januari na sasa atalazimika kutafuta uhamisho wa mkopo badala yake. (Sunday Telegraph)
Man United na Paris St-Germain wako tayari kulipa Yuro Pauni 60m (£52m) ili kumnunua kiungo wa kati wa Itali Nicolo Zaniolo, 20. (Il Messaggero - in Italian)
Man United ma Paris St-Germain wako tayari kulipa Yuro Pauni 60m (£52m) ili kumnunua kiungo wa kati wa Itali Nicolo Zaniolo, 20. (Il Messaggero - in Italian)
Mkufunzi wa Ugelgiji na meneja wa zamani wa Everton Roberto Martinez alitaka kuwa mkufunzi wa Tottenham baada ya Mauricio Pochettino kufutwa kazi. (Star on Sunday)
Borussia Dortmund inataka kumsaini mshambuliaji wa Tottenham na Jamhuri ya Ireland kaskazini mwenye umri wa miaka 17 Troy Parrott, huku pia klabu ya Ujerumani ya Bayern Munich ikiwa na hamu ya kutaka kumsajili . (Sunday Express)
Crystal Palace inakaribia kukamilisha ununuzi wa klabu hiyo wa dau la £215m . (Sun on Sunday)
Palace imewasiliana na Liverpool kuhusu makubaliano ya kumnunua mshambuliaji wa England Rhian Brewster mwenye umri wa miaka 19. (Football Insider)
Crystal palace ina hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Liverpool na England Rhia BrewsterHaki miliki ya picha
Lakini Aston Villa pia wana hamu ya kumsajili Brewster na wanaongoza katika kutafuta saini yake. (Sunday Mirror)
AC Milan inataka kumleta Zlatan Ibrahimovic, 38, katika klabu ya San Siro. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Sweden , ambaye kwa sasa hana klabu baada ya kuondoka katika klabu ya LA Galaxy, alishinda taji la Serie la mwaka 2010-11 Serie akiwa na klabu hiyo. (Calciomercato - in Italian)
Mkufunzi wa Bournemouth Eddie Howe anasema kwamba anataka winga Ryan Fraser kusalia lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anahusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal na Liverpool ameweka chaguo lake wazi. Kandarasi yake Fraser na timu yake inakamilika msimu ujao. (Sunday Mirror)
Ibrahimivic huenda akajiunga tena na klabu yake ya zamani Itali AC MIlan
Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, 32, anasema kuwa uhamisho wake katika klabu ya MLS ni uwezekano mzuri huku raia huyo wa Uruguay akihusishwa na klabu ya David Beckam Inter Miami.. (ESPN)
Mshambuliaji wa Inter Milan na Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, amesema kwamba alijua kwamba wakati wake katika klabu ya Man United umekamilika wakati mkufunzi Solskjaer alipoanza kumtumia katika wingi . (Football Italia)
Manchester United itapokea £850,000 kutoka kwa Juventus msimu ujao kama mojawapo ya makubaliano ambayo yalimfanya mshambuliaji wa zamani wa United Cristiano Ronaldo, 34, kujiunga na klabu hiyo ya Italia kutoka Real Madrid 2018. (Sun on Sunday)
Christiano Ronaldo aliichezea Man United klabu ya Kuelekja Real madrid
Arsenal wanakabiliana na Inter Milan katika kumsaini kinda mshambuliaji wa Flamengo na Brazil mwenye umri wa miaka 17 Reinier Jesus, 17. (Sun on Sunday)
Mario Balotelli analengwa na klabu ya Galatasaray. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na klabu yake ya nyumbani ya Brescia msimu uliopita. (Calciomercato - in Italian)
Newcastle United itamuuza kiungo wa kati wa South Korea Ki Sung-yueng, 30, in January. (Football Insider)

Post a Comment

0 Comments