Manchester City imeanza mazungumzo kuhusu mkataba mpya na mshambuliaji wa kimataifa wa England Raheem Sterling, 24. Mchezaji huyo anawindwa na Real Madrid
Mkufunzi wa Leipzig, Julian Nagelsmann na Jose Mourinho wanapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino, aliyefutwa kazi kama mkufunzi wa Tottenham. (Star)
Wengine ambao wamejumuishwa katika orodha hiyo ni Eddie Howe wa Bournemouth na Carlo Ancelotti wa Napoli ambao huenda wakapata kazi katika uwanja wa Tottenham Hotspur. (Sun)
Fidia itakayolipwa na Tottenham kwa kumfuta Pochettino na wafanyikazi wake huenda ikafikia £19.6m kiwango ambacho Manchester United ilimlipa Jose Mourinho na timu yake mwezi Disemba 2018. (Mirror)
Pochettino alifutwa kazi kufuatia malumbano kati yake na wachezaji katika chumba cha kubadilisha nguo hali ambayo ilifikia kiwango cha kuathiri utendakazi wake. (Mail)
Pochettino alikataa ombi la Daniel Levy la kumtaka ajiondoe hatua ambayo ilimfanya mwenyekiti wa Spurs chairman kumfuta kazi siku ya Jumanne. (Telegraph)
Red Devils huenda wakalipa hadi £85m kumsaini mshambuliaji wa Salzburg na Norway mzaliwa wa Leeds-Erling Braut Haaland, 19. (Standard)
Manchester United inamfuatilia mshambuliaji wa Reading Danny Loader, 19, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu. (Mirror)
Nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry, amepuuzilia mbali tetesi kuwa alitoa wito kwa Blues kutomsajili mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero kabla ahamie Manchester City. (Mirror)
Swansea na Stoke zinamtaka winga wa Celtic wa miaka 32- Jonny Hayes mkataba wake unapoelekea kukamilika. (Scottish Sun)
Robert Moreno anatarajiwa kutoa kauli yake kuhusu hatma yake kama kocha wa Uhispania baada ya hatua ya mkataba wake kuvunjwa. (AS - in Spanish)
Wachezaji wa Manchester United wameombwa kutotoka nje kwa zaidi ya dakika kumi watakaposafiri kucheza na FC Astana katika ligi ya Europa kutokana na hali ya baridi kali nchini Kazakhstan. (ESPN)
0 Comments