advertise with us

ADVERTISE HERE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO TAREHE 18-11-2019

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amepewa mwezi mmoja kunusuru kazi yake. (Sun)
Manchester City inatafakari uwezekano wa kuweka dau la kumnunua beki wa RB Leipzig Mfaransa Dayot Upamecano, 21, mwezi Januari. (90 Min)
Barcelona imekataa ofa ya karibu £13m, £17m kutoka kwa klabu ya ligi ya premia ya kumnuua kiungo wa kati wa Croatia Ivan Rakitic ambayo haijafikia thamani ya mchezaji huyo wa zamani wa Sevilla wa miaka, 31. (Sport)


Haki miliki ya picha

Crystal Palace inatarajiwa kuweka dau la £20m kumnunua mshambuliaji wa Celtic raia wa Ufaransa Odsonne Edouard, 21. (Sun)
Real Madrid na Barcelona huenda zikamwania beki wa Inter Milan kutoka Slovakia Milan Skriniar, 24, ambaye pia analengwa na Manchester United. (Corriere dello Sport)
Manchester United na Arsenal zinamfuatilia kipa wa Hartlepool wa miaka 17, Brad Young. (Sun)

Milan SkriniarHaki miliki ya picha

Manchester United inajiandaa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Tahith Chong huku klabu hiyo ikijaribu kudhibiti azma ya Juventus kumsaini kiungo huyo wa miaka 19. (Metro)
Chelsea inamtaka mshambuliaji wa Wigan wa miaka 17 - Muingereza Joe Gelhardt, ambaye pia anafuatiliwa na vilabu vya Manchester United, Manchester City, Liverpool, Tottenham na Everton. (Star)
Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 34, anasisitiza kuwa hana tatizo lolote na meneja Maurizio Sarri kufuatia matukio ya hivi karibuni yaliochangia kupumzishwa kwake. (Corriere dello Sport)

Haki miliki

Eric Abidal amethibitisha kuwa Barcelona wanamtaka kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22, kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 32. (Mundo Deportivo)
Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Abidal amemuunga mkono kocha Ernesto Valverde na kupinga madai kuwa klabu hiyo ya Catalan inamtafuta mshambuliaji mwingine. (Sport)
Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgii Michy Batshuayi, 26, anataka kusalia katika klabu hiyo na kupigania nafasi yake badala ya kuondoka mwezi Januari. (Sun)

Michy BatshuayiHaki miliki ya picha

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Genk na Norway Sander Berge, 21, amehusishwa na uhamisho wa Liverpool na Napoli, na amekiri kuwa kucheza katika uwanja wa Anfield itakuwa "ndoto". (Mirror)
Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Clive Allen, ambaye alicheza kidogo katika soka ya Marekani, anaamini mchezaji nyota wa sasa wa Spurs Harry Kane, 26, siku moja atajiunga na mchezo huo. (Star)

Post a Comment

0 Comments