BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO IJUMAA TAREHE 29-11-2019

Borussia Dortmund wako tayari kupokea ofa kutoka kwa winga wa England Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 19, mapema Januari.Sancho anahusishwa na Manchester United
Mchezaji wa zamani wa timu ya vijana wadogo ya Manchester City Sancho ndiye anayekosekana katika kikosi cha mashambulizi ambacho kitayafanya mashambulizi ya Liverpool ya kuogopwa zaidi kuliko kilivyo hata sasa, kwa mujibu wa mlinzi wa zamani wa Reds defender Jamie Carragher. (Daily mail)
Manchester United wameachana na mpango wao wa kumchukua mshambuliaji wa Juventus Mario Mandzukic, mwenye umri wa miaka 33 -rais wa Croasia (The Athletic, via Inside Futbol)
Borussia Dortmund wanamlenga Mandzukic pamoja na kiungo wa kati wa Juventus na Ujerumani Emre Can,25, Januari. (Sun)
Bruno Fernandes anayelengwa na Tottenham bado yuko makini kuondoka Sporting Lisbon, licha ya kusini mkataba mpya wa kipengele cha malipo ya pauni milioni 85. Kuna makubaliano yanayomruhusu kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 25 kutoka Ureno kuondoka iwapo malipo ya pauni milioni 60 yatapatikana (Mail)
Kylian Mbappe (kushoto) atajiunga na Real MadridHaki miliki ya picha
Mshindi wa Paris St-Germain na kombe la Dunia Kylian Mbappe, mwenye umri wa miaka 20, atajiunga na Real Madrid.(Le Parisien - in French)
Milan bado iko makini kusiani mkataba na difenda Mturuki Merih Demiral, mwenye umri wa miaka 21, ambae amekuwa akihusishwa na Manchester City pamoja na Arsenal. (Calciomercato)
Arsenal wanapanga kumlipa kiungo wa kati wa Real Madrid Mcolombia James Rodriguez pauni milioni 35 mwenye umri wa miaka 28, ambaye amekuwa akiaminiwa kuwa angependelea kuhamia katika Inter Milan au Paris St-Germain. (Eldesmarque - in Spanish)
Taarifa nyingine zinasema kuwa Rodriguez anataka kubakia katika Real Madrid na anajaribu kurejesha imani ya Zinedine Zidane kwake. (Marca)
Arsenal wanapanga kumlipa kiungo wa kati wa Real Madrid Mcolombia James Rodriguez pauni milioni 35
Kiungo wa kati wa Real Madrid -Fede Valverde, raia wa Uruguay mwenye umri wa miaka 21, amesaini mkataba utakaomuwezesha kuendelea kubaki katika klabu hiyo hadi mwaka 2025 wenye kipengele kinachomruhusu kuondoka kwa pauni £640m.(marca)
#Flamengo wameanza mazungumzo na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Diego Costa ambaye ni mzaliwa wa Brazil anayeichezea Atletico Madrid akiwa na umri wa miaka 31. (Goal.com)
Chelsea watafanya mazungumzo zaidi na winga wa Brazil Willian, mwenye umri wa miaka 31, juu ya hali yake ya siku zijazo baada ya mchezaji huyo kudai kuwa hajapewa mkataba mpya, licha ya klabu hiyo kusisitiza kuwa anao. (Telegraph)
Flamengo wameanza mazungumzo na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Diego Costa
Mlindalango wa Minnesota United Mcanada Dayne St. Clair, mwenye umri wa miaka 22, yuko tayari kufanya majaribio ya wiki mbili ya kimchezo katika Aston Villa.(Birmingham Mail)
Roy Hodgson anasema hatatoa hakikisho kwa Rhian Brewster, mchezaji wa timu ya Liverpool ya vijana walio chini ya umri wa miaka 21 -, mwenye umri wa miaka 19, la kucheza gemu katika Crystal Palace licha ya mazungumzo ya mkopo mweszi Januari. (Goal.com)
Chelsea watafanya mazungumzo zaidi na winga wa Brazil Willian, juu ya hali yake ya baadae ya kimchezoHaki miliki ya picha
Meneja wa Burnley Sean Dyche anasema ni mapema mno kujua ikiwa kiungo wa kati wa England Danny Drinkwater, mwenye umri wa miaka 29, atakuwa katika klabu hiyo baada ya mwezi Januari mwaka ujao. Drinkwater anacheza kwa mkopo kutoka Chelsea lakini bado hajacheza gemu ya timu ya kwanza ya Clarets tangu alipopata jeraha la fundo la mguu katika wakati alipohusika katika ugomvi kwenye kilabu cha pombe mwezi Septemba. (Sky Sports)
Mmiliki wa Hull Assem Allam anasisitiza kuwa klabu yake itakataa hadi pauni £20m kwa ajili ya kiungo wa safu ya mashambulizi Jarrod Bowen mwenye umri wa miaka 22- anayelengwa na Newcastle wakati wa dirisha la uhamisho wa wachezaji Januari.(Newcastle Chronicle)
Mlindalango wa West Ham mzaliwa wa Ghana Joseph Anang, mwenye umri wa miaka 19, amepandishwa darajaHaki miliki ya pichan
Mlindalango wa West Ham mzaliwa wa Ghana Joseph Anang, mwenye umri wa miaka 19, amepandishwa daraja na kufanya mazoezi na timu ya daraja la kwanza kabla ya mechi ya ligi kuu siku ya Jumamosi na Chelsea. (Football Insider)
Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson amesema Eagles walijaribu kusaini mkataba na mshambuliaji wa CSKA Moscow Mrusi Fedor Chalov, mwenye umri wa miaka 21, msimu uliopita lakini hawakuweza kuafikiana kuhusu mkataba. (Sport Witness)
Everton wameelekeza macho yao kwa mlinzi wa Nottingham Forest Muingereza Joe Worrall, mwenye umri wa miaka 22. (Football Insider)

Post a Comment

0 Comments