BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO ALHAMISI TAREHE 28- 11-2019

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi timu ya Ubelgiji Jan Vertonghen, mwenye umri wa miaka 32, bado yuko makini kujadili mkataba mpya na Tottenham kufuatia kuwasili kwa JoseMourinho 

Meneja wa Tottenham Mourinho ana matumaini ya kusaini mkataba na mlizi mwingine kutoka Ubelgiji Toby Alderweireld ambaye ana umri wa miaka 30. (Football.London)
Alderweireld, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, anajihisi kuwa mwenye''bahati'' kufanya kazi na Mourinho. (Talksport)
Patric Vierra anapangiwa kuwa Patrick Vieira (katikati)kama kocha mkuu wa klabu ya Inter MiamiHaki miliki ya picha
David Beckham anatarajia kumuajiri kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal na Ufaransa Patrick Vieira kama kocha mkuu wa klabu ya Inter Miami. (Telegraph)
Winga wa Borussia Dortmund Muingereza Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 19, anaaminiwa kuwa anapendelea kuhamia Real Madrid au Barcelona kuliko kuhamia Manchester United au Liverpool. (Star)
West Ham wanaweza kuangalia uwezekano wa kumrejesha David Moyes kama meneja wao kama watamfuta kazi Manuel Pellegrini. (London Evening Standard)
Jadon Sancho, anaaminiwa kupendelea zaidi kuhamia katika timu za Real na BarcelonaHaki miliki ya picha
Pep Guardiola bado anapendelea kubaki Manchester City na klabu hiyo imeazimia kuendelea kuwa na utawala ''endelevu'', kwa mujibu wa mwenyekiti wa klabu hiyo, Khaldoon Al Mubarak. (Goal.com)
Wakala wa mlinzi wa Leicester Caglar Soyuncu mwenye umri wa miaka 23 amepuuzilia mbali madai kwamba ana mpango wa kuhamia Arsenal, Manchester City au Galatasaray (Leicester Mercury)
Manchester United, Liverpool, Chelsea na Manchester City ni miongoni mwa timu saba zinazoongoza barani Ulaya kuwasiliana na wakala wa kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, mwenye umri wa miaka 20. (Bild, via Mail)
Pep Gardiola bado ataendelea kuwa Manchester CityHaki miliki ya picha
Mshambuliaji anayecheza katika klabu ya Rangers kwa mkopo, ambaye aliichezea England zamani katika nafasi hiyo Jermain Defoe, mwenye umri wa miaka 37, yuko tayari malipo yake yakatwe ili akamilishe mpango wake wa kuhama kutoka Bournemouth. (Football Insider)
Kiungo wa safu ya kati anayelengwa na Manchester United na Tottenham -Bruno Fernandes, Mreno mwenye umri wa miaka 25, amesaini mkataba mpya na Sporting Lisbon ambao unajumuisha kipengele kitakachomuwezesha kuondoka kwenye klabu hiyo kwa pauni milioni 20 hadi milioni 85. (Mirror)
Bruno Fernandes amesaini mkataba mpya na Sporting LisbonHaki miliki ya picha
Mkurugenzi wa michezo wa Real Valladolid Miguel Angel Gomez amekiri kuwa kufanya mazungumzo na mlinzi wa Ghana Mohammed Salisu, mwenye umri wa miaka 20, ambaye anakipengele cha kumuachilia cha euromilioni 12 na amekuwa akihusishwa na Manchester United na Everton. (Sport Witness)
Celtic wako tayari kumruhusu mchezaji wa safu ya kati mwenye umri wa miaka 21, kuondoka au hata kucheza kwa mkopo mwezi Januari . (Football Insider)
Muivory Coast Eboue Kouassi anaruhusiwa na Celtic kuhama timu hiyoHaki miliki ya picha
Mlinzi wa Ufaransa ambaye Barcelona inasema haimuhitaji- Samuel Umtiti, 26, angependa kumalizia taaluma yake ya soka katika Nou Camp lakini amedokeza kwamba anataka kupata nafasi katika timu ya soka ya daraja la kwanza. (Sport)
Manchester United hawapo sokoni tena kumtafuta mchezaji wa safu ya nyuma kushoto baada ya dharura ya kiungo wao wa mashambulizi Muingereza Brandon William. (Times - subscription required)
Wakala wa mshambuliaji wa River Plate striker Rafael Santos Borre amepuuzilia mbali taarifa kwamba Everton wamefanya dau kwa ajili ya Mcolombia huyo mwenye umri wa miaka 24. (Sport Witness)
Samuel Umtiti, 26, angependa kumalizia taaluma yake ya soka katika Nou CampHaki miliki ya picha
Leeds United wanamtafuta mchezaji atakayekaba nafasi ya Eddie Nketiah anayecheza kwa mkopo ikiwa Arsenal wataamua kumchukua tena Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 20 Januari. (Mirror)
Meneja wa Braga boss Ricardo Sa Pinto anaamini kwamba kocha wa Wolves Nuno Espirito Santo anastahili kuhusishwa na Arsenal lakini anahofia hali ya baadae ya rafiki yake Unai Emery. (Express and Star)
Uwanja mpya wa mazoezi wa Leicester' unakaribia kukamilika msimu ujao lakini hali ya hewa inawatatiza sana wajenzi wa uwanja huo. (Leicester Mercury)
Viongozi wa kidini wa Kibudha wameubariki uwanja mpya wa mazoezi kwa sherehe ya maombi. (Leicester Mercury)

Post a Comment

0 Comments