advertise with us

ADVERTISE HERE

TANZANIA YAVUNJA REKODI YA LEICESTER CITY KWA KUICHAKAZA VIBAYA MNO SUDAN KUSINI

Mwaka 2019 umekuwa ni mwaka wa neema kwa Tanzania upande wa mpira wa miguu kwani tumeshuhudia Taifa Stars ikicheza AFCON pale Misri. Timu ya U17 Serengeti Boys 


ilitwaa kombe la CECAFA U17 na Taifa Stars kufuzu CHAN 2020 huku ikianza vyema mchezo wake wa kwanza kufuzu AFCON 2021 kwa kushinda mabao 2-1. 

Lakini stori kubwa ya leo ni timu yaTaifa  ya Wanawake 'Kilimanjaro Queens' jana imeanza kwa kishindo michuano ya CECAFA uwanja wa Chamazi kwa ushindi wa mabao 9-0 dhidi ya Sudan Kusini.

Mchezo huu umevunja rekodi mbili kubwa kwenye soka . Ya kwanza ni ile ya klabu ya Leicester City kushinda mabao 9-0 dhidi ya Southhampton kwenye ligi kuu Uingereza na hakukuwa na timu nyingine iliyofanya hivyo duniani kwa kipindi hiki .


na rekodi ya pili mabao yaliyofungwa na Burundi mbele ya Zanzibar ambao walikubali kulala kwa mabao 5-0 uwanja wa Chamazi.

Mwanahamis Omari aliandika mabao yake matatu na kusepa na mpira wake akifunga mabao dakika ya 18,43 na 42, Donesia Minja alifunga bao lake moja matata kwa guu la kushoto dakika ya 33 huku Opa akipachika mabao mawili dakika ya 50 na 85 Stumai naye alipachika mawili dakika ya 48 na 52 aliyefunga bao moja mwingine alikuwa ni Juditha dakika ya 55.

Mchezo wa leo umeweka rekodi ya aina yake kwa Kilimanjaro Queens ambao ni mabingwa watetezi. Ripoti za mchezo ni kuwa Kilimanjaro Queens waliotea mara 23 na Sudan waliotea mara mbili pekee huku Mwanahamis Omary akikosa nafasi tatu za wazi kipindi cha kwanza kwa kile alichoeleza kuwa ni presha ya mchezo.

Post a Comment

0 Comments