Simba wametumia mitandao ya kijamii kusambaza ujumbe wa kuondokewa na nyota huyo aliyewahi kuitumikia pia timu ya Taifa la Tanzania. Kwenye taarifa hiyo simba waliandika
"Uongozi wa klabu ya Simba SC umepokea kwa masikitiko taarifa za kiungo wa zamani wa kimataifa wa klabu yetu Omari Gumbo ambaye alifariki ghafla jana jioni .
"Gumbo alipata kuwa makamu wa raisi wa klabu chini ya mwenyekiti Hassan Dalali alikuwa namba 6 hodari pia alipata kuichezea Taifa Stars. Tunatoa pole kwa ndugu ,jamaa na familia na watu wote walioguswa na msiba huu"
Mchezaji huyo atazikwa leo jijini Dar es salaam na taarifa kamili tutaitoa hivi karibuni.
0 Comments