advertise with us

ADVERTISE HERE

TAIFA STARS NA SIMBA ZAPATWA NA PIGO KUU

Timu ya Tanzania "Taifa Stars " imejikuta katika wakati mgumu kuelekea mechi na Libya itakayopigwa kesho jijini Tunis nchini Tunisia baada ya mchezaji mmoja kuachwa kikosini


Erasto Nyoni  aliyecheza kwa kiwango cha juu wakati Taifa Stars ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Guinea na atakaa nje kwa wiki kadhaa. Nyoni ameshindwa kusafiri na kikosi cha timu hiyo kwenda Tunisia kucheza dhidi ya Libya kutokana na majeraha ya goti.

Ndayiragije amesema kuwa, Nyoni ni muhimili mkubwa kwenye kikosi hicho haswa alikuwa anamtegemea kwenye mechi ya Jumanne lakini atapata mbadala wa haraka kwa vile kikosi hicho ni imara na uteuzi ni panama.

“Wachezaji wote wapo vizuri isipokuwa Nyoni, ambaye tumemuacha kutokana na majeraha ya goti aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Equatorial Guinea, tumemuacha ili afanyiwe vipimo na aendelee na matibabu,” alisema Ndayiragije, kocha wa zamani wa Mbao, KMC na Azam.

Kocha huyo raia wa Burundi, aliongeza kuwa, anayo njia mbadala ambayo ataitumia ili aweze kuziba pengo la mchezaji huyo wa Klabu ya Simba ambaye huenda akaiathiri timu hiyo kwenye kampeni za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwani ni tegemeo la Kocha Patrick Aussems.

Post a Comment

0 Comments