BETI NASI UTAJIRIKE

SUALA LA PATRICK AUSSEMS LAINGIA UKURASA MPYA SIMBA

Kamati ya maadili ya klabu ya Simba ikiongozwa na mwanasheria wa timu hiyo Michael Muhina ilikuwa na kikao kizito na kocha wa timu hiyo Patrick Aussems kilichodumu kwa 


muda wa saa 1 na dakika 40. Kikao hicho kilianza saa 11:00 jioni mpaka 12:40 jioni wakati kocha Aussems alipoonekana akitoka ukumbini akiongozana na msaidizi wa mwekezaji wa Simba Mohammed Dewji afahamikaye kwa jina la Babra Hernandez. 

Aussems alionekana akizungumza kwa kufoka huku akieleweshwa mambo kadhaa na Babra. Mazungumzo baina yao yalichukua dakika 3 huku Aussems akisubiri gari lake kumchukua na kuondoka .

Inaelezwa ajenda ya kikao hicho ni hatma ya Aussems ndani ya Simba anayetajwa kuondolewa kwenye timu hiyo. Kwa namna alivyotoka kwenye kika hicho Aussems anaonekana kutofurahishwa na maamuzi ya kikao hicho.

Post a Comment

0 Comments