BETI NASI UTAJIRIKE

SUALA LA DANTE LAENDELEA KUWA KIZUNGUMKUTI YANGA

Klabu ya Yanga imeshindwa kuelewana na mchezaji wa tim hiyo maarufu kama Dante. Mchezaji huyo anaidai klabu hiyo fedha ya usajili pamoja na malimbikizo ya mshahara


Mwanasheria  Alfred Mtawa anayemsimamia  beki wa Yanga Andrew Vicent 'Dante', amesema hatma ya suala la mteja wake litamalizwa na TFF baada ya pande mbili kushindwa kufikia mwafaka. Dante amekuwa nje ya kikosi cha Yanga tangu kuanza kwa msimu huu akishinikiza alipwe fedha za madai mbalimbali zinazofikia Tsh Milioni 54
-Inaelezwa awali TFF ilitoa muda kwa Yanga na Dante kukutana kumaliza sintofahamu iliyopo. Uongozi wa Yanga ulieleza kuwa tayari kumlipa mchezaji huyo kwa awamu, jambo ambalo yeye alilikataa. Mtawa amesema muda waliokuwa wamepewa na TFF kujadiliana umemalizika bila ya mwafaka kufikiwa hivyo wameiachia TFF kufanya uamuzi

Post a Comment

0 Comments