advertise with us

ADVERTISE HERE

SIRI YAFICHUKA YONDANI KUVULIWA UNAHODHA ,UGOMVI WA AJIBU NA YONDANI

Aliyekuwa kocha wa Yanga Mwingi Zahera ameendelea kutoboa siri mbalimbali za klabu hiyo. Zahera akiwa kwenye moja ya kituo cha redio jijini Dar es Salaam 



amemzungumzia beki kisiki Kelvin Yondani aliyewahi kuwa nahodha wa timu hiyo .Kocha huyo ambaye ni raia wa Congo, amesema alimvua Yondani sababu ya kuchelewa mazoezini jambo ambalo lilionesha si kiongozi.

"Nilimvua Yondani unahodha sababu ya utovu wa nidhamu, siwezi kuwa na nahodha ambaye anachelewa mazoezini, na wachezaji wenzake walisema hiyo ni tabia yake."

Aidha, kwa upande mwingine aliamua kumpa unahodha aliyekuwa mchezaji wa Yanga na sasa Simba, Ibrahim Ajibu na kumvua tena wiki kadhaa mbeleni.

Zahera ameeleza wakati anampa kitambaa Ajibu alikuwa mtulivu na alibadilika akawa na nidhamu.   maamuzi ya kumnyang'anya pia kitambaa kisha kumpa Papy Tshishimbi yalifikia baada ya mchezaji huyo kujiunga na Simba 

Post a Comment

0 Comments