BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA YAWEKA MASHARTI KWA TIMU ZINAZOTAKA HUDUMA YA WACHEZAJI WAKE

Klabu ya Simba inajiandaa kupunguza baadhi ya wachezaji kikosi hapo kwa kuwatoa kwa mikopo kwenda klabu nyingine na kupitia Afisa Mtendaji Senzo Mazingisa imetoa masharti 


kwa timu yoyote inayotaka wachezaji wake ni lazima iwe na uwezo wa kuwalipa mishahara wachezaji hao. Masingisa alinukuliwa akisema 

"Klabu nyingi zinataka kuchukua wachezaji wetu lakini zimekuwa zikishindwa kuwalipa mishahara na klabu ya Simba imekuwa ikilazimika kuwalipa wachezaji hao ,kwa sasa tumebadili utartibu wa kuwatoa wachezaji wetu kwa mkopo na tumezitaka timu hizo kutambua kwamba suala la kuwalipa wachezaji wanaozitumikia klabu hizo ni lao na si Simba hivyo anayemtaka mchezaji yeyote basi aelewe anatakiwa kumlipa mshahara pia"

Simba inajiandaa kusajili nyota wapya msimu huu wa dirisha dogo na kuwapunguza baadhi ya wachezaji klabuni hapo

Post a Comment

0 Comments