BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA YAOMBA MSAMAHA MASHABIKI NA KUAHIDI KUIMALIZA MBEYA CITY

Klabu ya Simba SC imeendelea na mazoezi asubuhi hii kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania dhidi ya Mbeya City mchezo utakaochezwa uwanja wa Uhuru Dar.



Mchezo wa mwisho Simba iliambulia kipigo cha bao 1-0 toka kwa Mwadui na kilikuwa ni kipigo cha kwanza  kwa timu hiyo  ligi kuu Tanzania.  Mbali na kipigo hicho Simba imeendelea kuongoza ligi kw pointi 18 ikicheza michezo 7 na kushinda 6 huku Kagere akifunga mabao 7 na mchezaji bora wa mwezi Septemba akifunga mabao 5.

Mara baada ya kurejea jijini Dar es salaam kocha wa timu hiyo Patric Aussems   alinukuliwa akiomba msamaha na kuahidi kufanya vizuri mechi zinazofuata. 

"Kupoteza kwetu haina maana kwamba tutaendelea kufungwa ni sehemu ya mpira na tuliyoyapata ni matokeo tumeyapokea.

"Kwa sasa tunachokifanya ni kuendelea kujipanga zaidi kwa ajili ya mechi zetu zinazofuata kwani ligi bado inaendelea,, kikubwa mashabiki watupe sapoti,
"

Hapo kesho Simba itacheza na mbeya City na tarehe 7 Novemba itacheza mchezo mwingine dhidi ya Prisons Mbeya 


Post a Comment

0 Comments