BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA WATIMIZA WALICHOTUMWA NA MANARA

Klabu ya Simba imefanikiwa kkupata ushindi wa mabao 4-0  dhidi ya Meya City mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. 



Simba walianza mchezo huo kwa kasi na dakika ya 9 walipata penati iliyosababishwa na miraji Athuman kuangushwa ndani ya Box . Penati hiyo ilipigwa na Kagere huku goli la pili likifungwa na kiungo mzambia Clatious Chama . Mpaka mpira unakwenda mapumziko Simba walikuwa wanaongoza kwa mabao mawili

Kipindi cha pili Simba ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Miraji na Kahata kuchukua nafasi yake. Shiboub aliipa tena Simba goli la 3 dakika ya 77 huku Deo Kanda akifunga bao la 4 dakika ya 86.

UJUMBE WA MANARA WAGEUKA KICHOCHEO 

"Nyie ni Klabu Bingwa ya taifa hili,nyie ni timu bora kupita zote Afrika Mashariki na ya kati kwa sasa! Nyie ni Wachezaji mnaoishi comfortable kuliko wachezaji wengine wowote ktk ukanda huu wa Afrika!!
Na nyie ndio Timu maarufu kupita zote ktk Zone hii, na mmetajwa na CAF ni klabu ya kumi na Sita bora Afrika nzima!!
Nadhan mtakuwa mmeelewa Wanasimba wanahitaji nn jioni ya leo hapa Uhuru Stadium,hususan baada ya kupoteza Kwenye last game!!
No Excuse today zaidi ya ushindi, hamtaeleweka na mm mtaninifanya niiasi insta kwa muda bila sababu!!!
Nipo huku Cairo nikiamini Mtatenda kitakachotendwa hapa ilipoishi Mitume mingi"
Kwa matokeo haya Simba inaendele kuwa nafasi ya kwanza kwenye ligi ikikusanya pointi 21  kwenye michezo 8 na meddie Kagere akiendelea kuwa namba 1 kwa wafungaji akifunga mabao 8 kwenye mechi 8,.


Post a Comment

0 Comments