Klabu ya Simba inajiandaa kuhamishia kambi yake ya mazoezi Bunju baada yya taarifa kusema uwanja huo umekamilika kwa asilimia 80 .
kupitia mwekezaji wake Mohammed Dewji taarifa zinasema kuwa kuna uwezekano ujenzi wa uwanja wa Bunju ukakamilika mwezi huu ama ujao.
Kauli hiyo imekuja kutokana na kuwepo kwa mvua ambazo zimesababisha ujenzi usimame kwa muda.
Mwenyekiti huyo wa bodi ya wakurugenzi amefunguka kuwa suala la uwekwaji wa kapeti lilishindikana ili kupisha mvua ambazo zilikuwa zinanyesha kwa kasi kubwa jijini Dar es Salaam.
Baada ya mvua hizo kusimama, zoezi hilo litaendelea tena na Mo ameeleza kufikia mwisho wa mwezi huu ama Disemba Simba wanaweza kuanza mazoezi ndani ya viwanja hivyo.
0 Comments