Mchezaji wa Manchester City na Ureno Bernado Silva amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuambiwa alipe kiasi cha Paundi 50,000 na kufungiwa mechi moja
dhidi ya Chelsea. Mchezaji huyo anashutumiwa kwa makosa ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji mwenzake wa Manchester City Benjamin Mendy kwa kumwekea picha yak na kikaragosi cheusi.
Siku ya jumatano FA walitangaza kumpiga fain na kumfungia nyota huyo kwa tweet aliyoiandika mwezi Septemba akiambatanisha picha ya utoto ya Mendy na kikaragosi cheusi kinachowakilisha Chocolate ya kihispania iitwayo Conguitos na baada ya dakika 46 aaliifuta tweet hiyo.
Kwa maelezo ya mmoja wa maafisa wa FA alimtetea Silva kwa kusema:
"Mchezaji huyo hakuposti kuonyesha ni ubaguzi wa rangi au kumtukana yeyote ,ni wazi kwamba tweet ile ilikuwa ni utani tu kati ya Silva na rafiki yake wa karibu Mendy . Ikumbukwe hakukuwa na usiri baina ya wachezaji hawa hasa kwenye mawasiliano. Picha hiyo ilikuwa kwenye mtandao wa kijamii wenye wafuasi 600,000 na wamekuwa wakimuheshimu mchezaji huyo"
Silva ni moja ya wachezaji wa Manchester City wanaopambana msimu huu kuhakikisha wanatwaa kombe la ligi kuu kwa mara nyingine tena. Kwa adhabu hiyo Silva ataukoa mchezo mgumu na muhimu dhidi ya Chelsea .
0 Comments