advertise with us

ADVERTISE HERE

SARRI AMTETEA CRISTIANO RONALDO

Kocha wa Juventus ameonekana hana tatizo na mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo baada ya kuondoka uwanjani hapo kabla ya  mechi haijamalizika baada ya kutolewa


 na nafasi yake kuchukuliwa na Dybala dakika ya 55 na kufanikiwa kufunga bao dakika ya 77 na mchezo kumalizka kwa Juventus kushinda bao 1-0.

Ronaldo alitolewa mchezo wa kwanza wiki  iliyopita kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Lokomotiv Moscow dakika ya 82 na nafasi yake kuchukuliwa na Douglas Costa . Hapo Jana alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Dybala.

Kocha Maurio Sarri alinukuliwa akimtetea

 "Tunatakiwa kumshukuru Ronaldo kwa kujitolea kwake kwenye mchezo huu maana alikuwa anasumbuliwa na mguu. Alijitahidi kucheza inavyopaswa lakini niliona hayuko sawa hivyo niliamua kumtoa,. Ni kawaida kwa mchezaji kutoka moja kwa moja bila kwenda benchi baada ya kutolewa uwanjan hasa anapokuwa na majeraha"

Sarri ameongeza mchezaji huyo hatapigwa faini yoyote na klabu hiyo kutokana na majeraha aliyokuwa nayo na uamuzi wa kutokaa benchi na wenzake ilikuwa sahihi.

Ronaldo anasumbuliwa na majeraha miguuni na kuna uwezejano akakosa michezo ya kimataifa ya kufuzu EURO 2020. 

Post a Comment

0 Comments