BETI NASI UTAJIRIKE

SAMATTA AWEKA REKODI MPYA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Nahodha wa taifa Stars na Genk Mbwana Ally Samatta ameibua hisia za watanzania usiku wa jana baada ya kuwafunga mabingwa watetezi wa kombe la ligi ya Mabingwa Ulaya 


Liverpool tena nyumbani kwao Anfield. Samatta anakuwa ni mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kuifunga Liverpool iliyosheheni wachezaji nyota zaidi duniani akiwamo Mo Salah, Sadio Mane , Van Dijk na Allison.

Liverpool walikuwa wakwanza kupata goli dakika ya 14 kupitia Wijnaldium. Samatta aliirudisha Genk mchezoni dakika ya 40 baada ya kupiga kichwa mpira wa kona na kufanya timu hizo kwenda mapumziko kwa mabao1-1.

Dakika ya 53 Oxlade aliipatia Liverpool bao la pili na mpaka dakika ya 90 Liverpool 2-1 Genk.



Post a Comment

0 Comments