Mshambuliaji hatari wa klabu ya KRC Genk na timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars " Mbwana Ally Samatta ametajwa kuwania tuzo za mchezaji bora kwa Afrika akichuana vikali
na Sadio Mane,Mohammed Salah na Aubemayang pamoja na wachezaji wengine kutoka Afrika wanaocheza soka la ulaya . CAF wametoa orodha ya wachezaji 30 waliofnya vizuri kwenye vilabu vyao na timu za Taifa huku Samatta akiwa ni mtanzania pekee aliyetokeza kwenye listi hiyo na anaendelea kuweka rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza kuwania tuzo za CAF kwa mara ya pili huku akifanya hivyo akiwa TP Mazembe.
Katika orodha hiyo iliyotolewa leo na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) wamo pia Mohamed Salah wa Misri (Liverpool), Piere-Emerick Aubameyang wa Gabon (Arsenal), Sadio Mane wa Senegal (Liverpool) na Riyad Mahrez wa Algeria (Manchester City).
Sherehe za tuzo hizo zitafanyika Januari 7, 2020 nchini Misri.
ORODHA KAMILI
Katika kipengele cha mchezaji bora wa mwaka ambako Mtanzania Mbwana Samatta yumo, orodha kamili hii hapa.
1. Achraf Hakimi - Morocco & Borussia Dortmund.
2. André Onana - Cameroon & Ajax
3. Baghdad Bounedjah – Algeria & Al-Sadd.
4. Carolus Andriamatsinoro - Madagascar & Al Adalah.
5. Denis Onyango - Uganda & Mamelodi Sundowns.
6. Eric Maxim Choupo Moting - Cameroon & PSG.
7. Ferjani Sassi - Tunisia & Zamalek.
8. Hakim Ziyech - Morocco & Ajax.
9. Idrissa Gueye - Senegal & Paris Saint-Germain.
10. Ismail Bennacer - Algeria & AC Milan.
11. Jordan Ayew - Ghana & Crystal Palace
12. Kalidou Koulibaly - Senegal & Napoli.
13. Kodjo Fo Doh Laba - Togo & Al Ain.
14. Mahmoud Hassan"Trezeguet" - Egypt & Aston Villa.
15. Mbwana Samatta - Tanzania & Genk.
16. Mohamed Salah - Egypt & Liverpool.
17. Moussa Marega - Mali & Porto.
18. Naby Keita - Guinea & Liverpool.
19. Nicolas Pepe - Côte d'Ivoire & Arsenal.
20. Odion Ighalo - Nigeria & Shanghai Shenhua.
21. Percy Tau - South Africa & Club Brugge.
22. Pierre-Emerick Aubameyang - Gabon & Arsenal.
23. Riyad Mahrez - Algeria & Manchester City.
24. Sadio Mane - Senegal & Liverpool.
25. Taha Yassine Khenissi - Tunisia & Esperance.
26. Thomas Teye Partey - Ghana & Atlético Madrid.
27. Victor Osimhen - Nigeria & Lille.
28. Wilfred Ndidi - Nigeria & Leicester City.
29. Wilfried Zaha - Côte d'Ivoire & Crystal Palace.
30. Youcef Belaili - Algeria & Ahli Jeddah.
0 Comments