Kuelekea mchezo wa kufuzu Afcon mwaka 2021 nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta amesema kuwa morali ya wachezaji ni kubwa kuelekea kwenye mchezo wa kufuzu Afcon
Ijumaa Novemba 15 dhidi ya Equatorial Guinea.Samatta amesema kuwa kazi ni ngumu kwa timu kutafuta matokeo ila kikubwa watafuata mbinu walizopewa na mwalimu kushinda.
"Haitakuwa kazi nyepesi kwani ushindani ni mkubwa, kila timu inahitaji ushindii nasi pia tunahitaji matokeo chanya.
"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti nasi tutapambana ndani ya uwanja ili yasijirudie ya msimu uliopita tulipolazimisha sare nyumbani," amesema.
0 Comments