BETI NASI UTAJIRIKE

ROMELU LUKAKU NI YULE YULE ILA MANCHESTER UNITED ILIKWAMA WAPI KUMTUMIA

Aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United na sasa anaitumikia Inter milan Romelu Lukaku ameendelea kuwa mwiba mkali kwa mabeki wa Serie A na Ligi ya Mabingwa ulayaLukaku amekuwa na kwango cha juu sana tangu alipojiunga na Inter milan akitokea Manchester United. Kupitia uwepo wake timu hiyo imefanikiwa kupata pointi 7 sawa na Dortmund kwenye kundi F wakipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Slavia Praha.

Kwenye mchezo huo Lukaku alifunga bao 1 huku akisaidia upatikanaji wa bao jingine kupitia Martinez. Mbali na kufanya vizuri ligi ya mabingwa Ulaya mchezaji huyo amefanya vizuri kwenye ligi kuu italy kwa kufunga mabao 10 na kushika nafasi ya pili kwa ufungaji akicheza michezo 13.

Lukaku ameisaidia Inter Milan kushika nafasi ya pili ligi kuu Italia "SERIE A" kwenye michezo 13 na kupata pointi 34 nyuma ya vinara Juventus wenye pointi 35. 

Kwa Upande Manchester United  

Machester United imeendelea kuwa na wakati mgumu msimu a 2019/20 ikicheza michezo 13 ikishinda 4 sare 5 na vipigo 4 huku ikishika nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi na kufunga mabao 19 ikiruhusu mabao 15. 

Manchester United ni kama imekosa mshambuliaji wa kati kwani Ole Gunnar amekuwa akiwatumia nyota kadhaa akiwemo Rashford,Lingard na Martial bila mafanikio yoyote .

Swali linakuja je ni kwanini Ole Gunnar alimwondoa Lukaku kikosini ilihali alifanya vvizuri kwa misimu miwili iliyopita akiwa na Jose Mourinho? Hizi ni takwimu za Lukaku akiitumikia Manchester United.

 Hizi hapa takwimu za Lukaku akiwa na Manchester United kwenye michuano mbali mbali ikiwemo UEFA na Ligi kuu Uingereza (EPL)


Post a Comment

0 Comments