ads

adds

RIPOTI: MATOKEO YA LIGI KUU MECHI ZA YANGA,AZAM NA KAGERA SUGAR

Klabu ya Yanga imetangaza kurejea mbio za ubingwa baada ya kupata ushindi wa ugenini katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara 


baada ya kuwachapa wenyeji, Ndanda FC 1-0 jioni ya leo .

 Kagera Sugar imeendelea kufanya vizuri baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, KMC Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.


Mabao ya Kagera Sugar inayofundishwa na Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Mexime yamefungwa na viugno Awesu Awesu kwa penlati dakkika ya 25 na Peter Mwalyanzi dakika ya 48, wakati la KMC ya kocha Mganda, Jackson Mayanja limefungwa na Serge Nogues dakika ya 86.

Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.


Ushindi huo wa kwanza chini ya Mromania Aristica Cioaba tangu arejeshwe unaifanya Azam FC ifikishe pointi 13 baada ya kucheza mechi saba na kupanda hadi nafasi ya 11 kutoka ya 14.

Mabao ya Azam FC katika mchezo wa leo yamefungwa na kiungo Idd Suleiman ‘Nado’ dakika ya pili akimalizia pasi ya Mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma na beki Mganda, Nicolas Wadada dakika ya 23 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mzambia Obrey Chirwa.

Post a Comment

0 Comments