aliechezesha mchezo huo afahamikae kwa jina la Chizinga Mwi na utaifa wake ni Malawi. Mchezo uliopigwa nchini Tunisia na refa huyo kusababisha Stars kupoteza mchezo wake wa kwanza kati ya michezo 6 inayopaswa kucheza hatua za makundi.
Taifa Stars ilikuwa ya kwanza kufunga bao dakika ya 18 kwa mkwaju wa penalti kupitia Mbwana Samata baada ya Msuva kuchezewa rafu.
Dakika ya 68 mwamuzi alitoa penalti yenye utata kwa Libya jambo lililowavunja moyo wachezaji wa Taifa Stars kwenye mchezo huo na bao likapachikwa na Sand Masoud dakika ya 68 ambaye alipiga penalti.
Zikiwa zimesalia dakika 9 mpira kumalizika mchezaji wa Libya Anias Saltou aliandika bao la pili akiwa ndani ya 18 kutokana na safu ya ulinzi kufanya makosa ya wazi.
Dakika ya 87 mchezaji wa Libya Hamdou Mohamed alionyeshwa kadi nyekundu na kuondolewa uwanjani.
0 Comments