BETI NASI UTAJIRIKE

REAL MADRID NA BARCELONA ZAMPIGIA HESABU STAA WA ARSENAL

Klabu  za Barcelona na Real Madrid zimeingia katika vita kuwania saini ya mshambuliaji wa Gabon na Arsenal Pierre Aubemayang. Mshambuliaji huyo alihusishwa na kuhamia Manchester United lakini klabu hizo za Hispania zimeonekana kumuwinda nyota huyo kwa udi na uvumba . Klabu ya Arsenal bado haijasema chochote kuhusiana na nyota huyo aliyekuwa mfungaji bora wa msimu wa 2018/19 akifungana na Sadio Mane na Mohammed Salah wa Liverpool na kuweka rekodi ya kuwa wachezaji watatu kutoka Africa kutwaa tuzo hiyo.

Aubemayang ametajwa kuwania tuzo za mchezaji bora Afrika akichuana na Mbwana Samata wa Tanzania na KRC Genk. Mchezaji huyo anaweza kuondoka klabuni hapo kutokana na mwenendo mbovu wa klabu hiyo na kutocheza Ligi ya Mabingwa itakuwa ni moja ya sababu kuu.

Post a Comment

0 Comments